Hissene Habre, anashitakiwa kwa makosa ya kukiuka haki za binadamu wakati wa utawala wake mnano miaka ya 1982 - 1990.Kesi hii dhidi ya Hissene Hebre ilifunguliwa na raia wa Ubeligiji mwenye asili ya Chad kwa madai kuwa wakati wa utawala wa Hissene Hebre watu wapatao 40,000 waliteswa na hata wengine kupoteza maisha.Hissene Hebre yupo ukimbizini nchi Senegal ambako alikimbilia baada ya utawala wake kuondolewa.
20 Julai 2012 - 19:30
Msimbo wa Habari: 330618
ABNA inatuarifu kuwa:Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia makosa ya ukiukaji wahaki za binadamu iliyoko Ubeligiji, imetaka aliyekuwa rais wa Chad akamatwe ili ajibu mashitaka ya kukiuka haki za binadamu.